25
Nov

TFS YASHIRIKI MAZOEZI YA PAMOJA YA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA

Jeshi la Uhifadhi la Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) limeshiriki katika mazoezi ya pamoja ya vyombo vya ulinzi na usalama nchini, yaliyolenga kuimarisha ushirikiano, utayari na uwezo wa taasisi katika kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Uzinduzi wa mazoezi hayo umefanyika Jana ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Patrobas Katambi, ukihudhuriwa na viongozi wa vyombo na taasisi mbalimbali za ulinzi na usalama, wakiwemo viongozi wa Jeshi la Uhifadhi.

Ushiriki wa TFS unaonesha dhamira ya taasisi katika kuimarisha ushirikiano na vyombo vingine vya ulinzi na usalama, pamoja na kujenga uwezo, nidhamu na utayari wa kukabiliana na changamoto mbalimbali katika utekelezaji wa majukumu ya kulinda rasilimali za misitu na kuhakikisha usalama.