02
Nov
SEMINA ELEKEZI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA
Pichani ni viongozi na watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), wakiwemo maafisa na askari kutoka Makao Makuu na Kanda ya Kati, Dodoma, wakiongozwa na Naibu Kamishna wa Uhifadhi, DCC Emmanuel Wilfred Kiboko, wakishiriki semina elekezi ya siku mbili inayolenga kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa na kuzuia vitendo vya rushwa mahali pa kazi.
Katika semina hiyo, mada mbalimbali zinawasilishwa, zikiwemo Mkakati wa TFS wa Kupambana na Rushwa wa mwaka 2023/2024 hadi 2029/2030, taratibu za mashauri ya nidhamu na maadili kwa watumishi wa TFS, pamoja na vitendo vya rushwa na ubadhirifu vinavyoweza kujitokeza katika utekelezaji wa majukumu ya watumishi.
Semina hiyo itafunguliwa na kufungwa rasmi na Kamishna wa Uhifadhi wa TFS, Profesa Dos Santos Silayo, kesho tarehe 3 Novemba 2026, katika ukumbi wa Hoteli ya Best Western, jijini Dodoma.