16
Nov
TIMU YA TFS YATINGA ROBO FAINALI MASHINDANO YA SHIMMUTA
Morogoro, Novemba 16, 2026 – Timu ya mpira wa pete ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya mashindano ya SHIMMUTA baada ya kuichapa timu ya Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) kwa magoli 61-37.
Mchezo huo umechezwa leo katika Uwanja wa Morogoro Sekondari, ambapo timu zote zilionesha ushindani, huku TFS ikitawala mchezo na kupata ushindi huo muhimu ulioiwezesha kusonga mbele katika michuano hiyo.
Kwa ushindi huo, TFS sasa inasubiri kucheza na mshindi wa mchezo kati ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Arusha (AUWASA) na Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Afrika ya Nelson Mandela (NM-AIST) katika hatua ya robo