19
Feb
NAIBU WAZIRIWA MALIASILI MHE.CHANDE AONGOZA HAFLA YA UTOAJI TUZO TAFORI
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb.), ameongoza hafla ya utoaji wa Tuzo na Zawadi za Heshima zilizoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) kupitia Menejimenti ya Utumishi, kwa ajili ya kutambua na kuthamini utendaji wa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi kwa kipindi cha miaka mitatu.
Katika hafla hiyo, viongozi mbalimbali wa Wizara ya Maliasili na Utalii walitunukiwa zawadi maalum, akiwemo Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo, aliyekuwa miongoni mwa waliopokea tuzo kwa mchango wao katika kuimarisha sekta ya misitu na uhifadhi.
TAFORI pia iliwatunuku Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Utalii, huku baadhi yao wakiwakilishwa na watendaji wao.
Hizi ni baadhi ya picha za matukio zikimuonesha Mhe. Chande akikabidhi tuzo kwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TAFORI, katika hafla iliyoangazia uwajibikaji, ufanisi na mchango wa viongozi katika maendeleo ya rasilimali za misitu nchini.