03
Nov
TFS Watumia Michezo Kuhamasisha Uhifadhi
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania umeaandaa bonanza la michezo ambalo limewakutanisha takribani watumishi 251 kutoka katika kanda zinazosimamiwa na TFS kwa lengo la kuwaweka karibu na kujenga zaidi ushirikiano baina yao ambalo limeanza Novemba 1, 2024 uwanja wa Agha Khan jijini Arusha.
Bonanza hilo limezinduliwa na SACC Peter Mwakosya(Mhasibu Mkuu) kwa niaba ya Kamishna wa Uhifadhi TFS Prof Dos Santos Silayo ambapo amesema kuwa Wakala umeona ni muhimu kufanya bonanza hili ili kuweka chachu kwa watumishi kufanya mazoezi mara kwa mara ili kujenga afya na kuondokana na magonjwa yasiambukiza.
Amewakumbusha kuwa wanatakiwa kubadili mtindo wa maisha kwa kuangalia aina bora za vyakula na kuondokana na matumizi ya vilevi yaliyopitiliza na kuhakikisha kila mmoja anafuata ushauri wa madaktari ili kufanya afya kuwa nzuri wakati wote. Pamoja na vilezi vingine.
Ameendelea kuwasisitiza kuwa michezo ni sehemu ya kazi hivyo kuhakikisha makamanda wote wa kanda na mashamba kupanga bajeti ili watumishi waweze kushiriki michezo mbalimbali itakayofanyika.
Amewataka kuendelea kuwa waadilifu, kuongeza weledi na bidii zaidi katika utekelezaji wa majukumu ya kazi ya kila siku kwa kwahudumia wateja na kwa kuzingatia sheria na miongozo iliyopo.
Bonanza la TFS SPORTS BONANZA limeanza tarehe Novemba 1, 2024 na litahitimishwa Novemba 4, 2024 na litakuwa likifanyika kila mwaka ili kujenga afya na kuwakutanisha wahifadhi kuboresha mahusiano na kuongeza ushirikiano zaidi.