
06
Feb
Wataalamu wa sekta misitu,mifugo,kilimo,nyuki,mbegu za miti kujadili mikakati kuhusu mradi wa Miombo
Dodoma-03 Februari 2025
Wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais,Wizara ya Maliasili na na Utalii na Wizara ya Kilimo,mifugo wamekutana jijini Dodoma kwenye kikao kazi cha kupitia na kujadili mawasilisho mbalimbali ya kitaalamu kuhusu mikakati shirikishi ya sekta zao kwa ufadhili wa mradi ambao kwa Tanzania unatekelezwa katika mikoa ya Tabora(Kaliua na Urambo)na Katavi(Mlele).
Akifungua kikao hicho Mkurugenzi msaidizi wa misitu na nyuki Daniel Pancras amesema mradi huo ni muhimu sana kwa usitawi wa misitu ya miombo ya nyandakame ambayo imeathiriwa kwa kiasi kikubwa na shughuli za kinadamu kwenye mikoa husika.
"Mradi huu ni muhimu,lakini muhimu ni hili la kushirikisha idara za kisekta kwa kuwa bila ushirikiano wa kisekta ni ngumu kufikia malengo ya mradi huu, shughuli za kinadamu ndiyo zimeathiri misitu ya miombo hivyo ni muhimu sana kushirikisha wananchi,idara, taasisi na mamlaka nyingine ili kuwa na malengo ya pamoja"Pancras.Kikubwa kuwa na mikakati ambayo inatambua umuhimu wa sekta nyingine.
Akizungumza kwa niaba ya Kamishna wa uhifadhi TFS Kamishina Msaidizi mwandimizi Dkt Hamza Kateti ameeleza namna ambavyo misitu ya miombo ya nyandakame imekuwa kielelezo cha mikoa ya Tabora na Katavi kwa miaka mingi.
"Kwa sisi ambao tumefanya uhifadhi kwa muda mrefu kidogo tunaweza kukumbuka Tabora ya zamani na miombo yake,siyo Tabora pekee ni maeneo mengi lakini miombo ni kielelezo kizuri cha uhifadhi hivyo mradi huu ukitekelezwa vizuri unaweza kurejesha ile Tabora tunayoijua wengi"Dkt Kateti.
Naye Bw Thimotheo Mande mratibu wa mkataba wa kupambana na Jangwa na Ukame -UNCCD kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais amefafanua namna ambavyo mradi huo unahusiana na miradi mingine ya kimataifa,kikanda na ndani ya nchi ambapo amesisitiza umhimu wa kuhakikisha miradi ya kiuhifadhi na kimazingira inatekelezwa kwa ushirikiano wa kisekta kama ambavyo mradi huu unahusisha WADAu
Katika kikao kazi hicho pamoja na Mambo mengine Mratibu wa mradi huo Kamishna Msaidizi wa uhifadhi Zainabu Bungwa kutoka Wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS)amewataka washiriki kuchangia hoja na kutoa maoni kwa kila wasilisho la Rasimu ya mkakati wa sẽkata husika ili kurahisisha utekelezaji wa mradi huo muhimu. Kikubwa Bungwa amewajulisha washiriki kuwa mradi huu ni mradi wa mfano wa ushirikiano wa Sekta na vivyo Hivyo mikakati shirikishi iwe ya mfano kwa mradi huu.
Kikao hicho kimehudhuriwa na mtaalamu mwelekezi Mr Juma Mgoo,Mtaalamu kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam Dr.Manoko ; SACC Husein Msuya na makundi ya maafisa wa kilimo,mifugo,misitu,nyuki ; mbegu za miti