04
Jul
Kikao kuhusu Mradi wa usimamizi shirikishi wa Misitu ya Miombo Wilayani Kaliua
Naibu Kamishna wa uhifadhi Caroline Malundo amakalisha ziara ya kikazi TFS kanda ya magharibi ambapo tarehe 18/04/2024 amefanya kikao cha pamoja na wadau wa uhifadhi wilaya kaliua kilichoongozwa na Mkuu wa wilaya Mhe Rashid Chuachua na kuhudhuriwa pia na mkurugenzi mtendaji wa halimashauri ya kaliua Bw Jerry Diamond Mwaga.
Kikao hicho kimejadili mradi wa usimamizi shirikishi wa misitu ya miombo maana yake, malengo yake na manufaa yake kwa ustawi wa Tanzania.
Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Mratibu wa mradi SACC Zainabu Bungwa, Kamanda wa TFS kanda ya magharibi SACC Lebrantino Mgiye na maafisa wengine kutoka TFS makao makuu Dodoma pamoja na DFC kaliua.
Mradi wa usimamizi shirikishi wa misitu ya miombo Tanzania unatekelezwa chini ya ofisi ya Makamu wa Rais kupitia shirika la kilimo na chakula duniani FAO kwa ufadhili wa mfuko wa mazingira duniani GEF ambapo TFS ni msimamizi mkuu wa utekelezaji wa mradi huo Tanzania.
DCC Caroline Malundo akitoa maelezo ya awali mbele ya Mkuu wa wilaya ya Kaliua kabla ya kikao na wadau wa uhifadhi.