25
Sep
VIONGOZI WAPATA TIBA YA APITHERAPY KATIKA BANDA LA TFS
VIONGOZI WAPATA TIBA YA APITHERAPY KATIKA BANDA LA TFS
Na Mwandishi Wetu, Arusha
VIONGOZI mbalimbali waliotembelea banda la Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) katika ukumbi wa Ngurdoto, Arusha jana Septemba 26,2026, wamepatiwa huduma ya tiba kwa kutumia bidhaa na huduma zitokanazo na nyuki, maarufu kama Apitherapy.
Miongoni mwa viongozi hao ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Dk Jim Yonazi, na Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge Vinara wa Ufuatiliaji, Tathmini na Ujifunzaji, Mhandisi Mwanaisha Ulenge.
Baada ya kupata huduma hiyo, viongozi hao waliipongeza TFS kwa kuendelea kutoa huduma kwa wananchi kupitia shughuli zake za uhifadhi wa misitu, nyuki na matumizi endelevu ya rasilimali za misitu.
Aidha, waliihimiza TFS kuendelea kuimarisha utendaji wake na kutoa huduma zenye tija kwa wananchi, sambamba na kuongeza uelewa kuhusu fursa zinazotokana na uhifadhi wa misitu na rasilimali za nyuki.
Viongozi hao walipokelewa na Meneja wa Mipango na Masoko wa TFS, ACC Neema Mbise, aliyewapatia elimu kuhusu shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Wakala katika uhifadhi wa misitu na maendeleo ya sekta ya nyuki.
Baada ya ziara hiyo, viongozi hao walikabidhiwa zawadi maalumu kutoka TFS kama sehemu ya kuwakumbusha umuhimu wa uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali za misitu na nyuki.