02
Oct

SERENGERTI RALLY OF TANZANIA 2026 YAZINDULIWA RASMI MOROGORO

Mkuu wa wilaya ya Morogoro mjini Mhe Mussa Kilakala amezindua rasmi mashindano ya mbio za magari ya serenget Rally of Tanzania  yanayotaraji kuanza kutimua vumbi katika msitu wa shamba la miti Morogoro mapema siku ya kesho

Mhe Kilakala amehimiza suala la usalama kwa washiriki na watazamajj sambamba na utunzaji wa mazingira wakati wote wa mashindano hayo

Aidha akizungumza katika uzinduzi huo Naibu Kamishna anatesimamia kurugenzi ya uzalishaji mbegu za miti Dkt Hamza Kateti amesema TFS itaendelea kutunza mazingira ambayo ndiyo chachu ya mashindano hayo kufanyika Morogoro, aidha amewataka wananchi wote kujitokeza na kufanya utalii ikolojia katika hifadhi mbalimbali zinazopatikana mkoan Morogoro ambazo pia zinasimamiwa na TFS