
20
Sep
TFS YAKABIDHI VIFAA VYA TEHAMA KWA SHULE ZA MSINGI MBILI
Tunduma – Songwe: Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania – TFS umekabidhi Kompyuta 34 na Meza 20 na viti 40 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 40 kwa shule mbili za msingi za Halmashauri ya mji wa Tunduma mkoani Songwe ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Serikali za kujenga na kuboresha miundombinu ya madarasa nchini.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo vya TEHAMA Kamishna wa Uhifadhi TFS, Prof. Dos Santos Silayo mwishoni mwa wiki (Januari 20, 2022) anasema ili uweze kufikisha elimu ya uhifadhi kwa haraka kwa mtu yoyote TEHAMA haiepukiki na kwa sababu hiyo wameam