Resources » News and Events

UUZAJI WA MITI YA MISAJI KWA NJIA YA MNADA WA KIELEKTRONIKI

MMOJA WA WANUNUZI WA TEAK AKIPIMA GOGO LA MTI ALIOVUNA KUTOKA KWENYE SHAMBA LA MTIBWA

UUZAJI WA MITI YA MISAJI KWA NJIA YA MNADA WA KIELEKTRONIKI

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) utauza miti aina ya misaji yenye jumla ya  meta za ujazo 13,235.27 iliyopo katika Shamba la miti Mtibwa, Turiani Mkoani Morogoro    na Shamba la miti Longuza, Muheza Mkoani Tanga. Jumla ya meta za ujazo 7980.91 na 5254.36 zitauzwa katika shamba la mitiMtibwa na Longuza mtawalia.

Miti itauzwa kwa njia ya mnada wa kielektroniki kwa kuzingatia Kanuni ya 31 (ii) ya Kanuni za Misitu za Mwaka 2004. Mnada huu utafanyika siku ya Alhamisi tarehe 26 Januari, 2023 kwa Shamba la Miti Mtibwa na Ijumaa tarehe 27 Januari, 2023 kwa Shamba la Miti Longuza. Muda wa kuanza mnada itakuwa saa moja kamili (01:00) asubuhi hadi saa kumi kamili (10:00) jioni.

Ili kushiriki kwenye mnada, mshiriki atatakiwa kujisajili kupitia anuani ifuatayohttp://mis.tfs.go.tz/e-auction kuanzia tarehe ya tangazo hili hadi saa sita kamili (6:00) usiku wa tarehe 24 Januari, 2023 siku ya Jumanne. Kwa ajili ya msaada wa usajili, wasiliana na: +255713 335 926 or +255 766 857 062.

 

SALES OF STANDING TEAK TREES BY ELECTRONIC AUCTION

The Tanzania Forest Service (TFS) Agency will sell standing trees with 13,235.27 m3 located at Mtibwa Forest Plantation, Turiani, in Morogoro Region and Longuza Forest Plantation, Muheza, inTanga Region. A total of 7980.91 and 5254.36    will be sold at Mtibwa and Longuza Forest Plantations,respectively.

Trees will be sold through electronic auction in accordance with Regulation                   31 (ii) of the Forest Regulations (2004). The auction will take place on Thursday, 26th January 2023, for Mtibwa Forest Plantation and Friday, 27th  January 2023, for Longuza Forest Plantation. The auction will start from 07:00 hrs. until 16:00 hrs. in the evening.

In order to participate in the auction, the participant will be required to register through thefollowing address http://mis.tfs.go.tz/e-auction from the date of this advertisement until midnight (00:00Hrs) of 24th January 2023 on Tuesday. For online registration assistance, contact +255713 335 926 or +255 766 857 062.

Downloads File: