Resources » News and Events

WAHIFADHI 47 WAHITIMU MAFUNZO YA UONGOZI WA KIJESHI JIJINI ARUSHA

Kamishna wa Uhifadhi TFS Prof. Dos Santos Silayo (aliyesimama) akimueleza jinsi walivyojipanga kulinda rasilimali misitu nchini Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Brigedia Jenerali Mbaraka Mkeremy  (aliyekaa)Kamishna wa Uhifadhi TFS Prof. Dos Santos Silayo (aliyesimama) akimueleza jinsi walivyojipanga kulinda rasilimali misitu nchini Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Brigedia Jenerali Mbaraka Mkeremy (aliyekaa)

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Brigedia Jenerali Mbaraka Naziad Mkeremy amewataka wahitimu 47 wa mafunzo ya uongozi wa kijeshi kwa viongozi wa TFS kuhakikisha wanafanya kazi kwa weledi ikiwemo kukabiliana na changamoto za uharibifu wa misitu.

Aidha amesisitiza watumie mafunzo hayo kukabiliaa na changamoto mbalimbali za kiutendaji na kuimarisha weledi katika utekelezaji wa shughuli za uhifadhi ikiwemo kulinda amani ya nchi kwa mfumo mpya wa kijeshi.

Akizungumza wakati wa kuhitimisha mafunzo ya viongozi kutoka makao makuu na vituo mbalimbali vya TFS ikiwemo kanda za uhifadhi, mashamba ya miti, kituo cha mbegu na mashamba ya nyuki Brigedia Jenerali, Mkeremy amesisitiza uzalendo kwa viongozi hao ili kutetea nchi na kulinda rasilimali zilizopo.

Alisema anaamini mafunzo hayo yalete mabadiliko ya kiutendaji katika vituo vya kazi vya viongozi hao ikiwemo kubainisha masuala muhimu ya kufanyia kazi ili kuleta mabadiliko na ufanisi mahali pa kazi ikiwemo mfumo wa kufuatilia utekelezaji wa mafunzo waliyopata kabla ya kupata uongozi.

“Kila kiongozi atekeleze majukumu yake na awe mwalimu kwa wasaidizi wake kwa kuonesha mfano wa namna utekelezaji wa majukumu unavyopaswa kuwa. Kiongozi mzuri anapaswa kutatua changamoto zilizopo katika eneo lake na kama kiongozi uwe mstari wa mbele katika kubainisha masala muhimu ya kuendelea kufanyia kazi na kuyatolea taarifa ili menegement ya Jeshi iandae mkakati wa utekelezaji,”

“Bodi inatarajia kuona mabadiliko ya kiutendaii vanavoendana na mafunzo haya. Napenda kusisitiza kila mmoja wenu kutekeleza wajibu wake kwa nafasi aliyopewa kwa kuzingatia taratibu za Jeshi mlizofundishwa. Kila mmoja kwenye kituo chake ahakikishe maafisa na askari wanatekeleza kwa vitendo masuala yote mliyofundishwa na kuwe na mfumo wa kupima ufanisi wa utekelezaji.” anasisitiza Brigedia Jenerali Mkeremy.

Aliishukuru serikali kwa kuendela kuijengea uwezo TFS na kusimamia kidete ajenda ya uhifadhi kwa kuongeza ajira za wahifadhi na ununuzi wa vitendea kazi ili yale yaliyoridhishwa yaendelee kuridhishwa na vizazi vijavyo.

Katika hatua nyingine jumla ya wahifadhi 11 wamehuishwa vyeo kuendana muundo wa taasisi  ambapo sasa wanakuwa Makamishna wasaidizi waandamizi ambapo awali walikuwa ni Makamishna wa uhifadhi wasaidizi. Aidha, Maafisa Wakuu wawili waandamizi wakipandishwa cheo kuwa Wahifadhi Wakuu.

Kamishna wa Uhifadhi TFS Prof. Dos Santos Silayo anasema kupitia mafunzo hayo wahifadhi wataweza kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiutendaji katika mfumo wa kijeshi katika nyanja za uongozi wa kijeshi, intelijensia, itifaki, upelelezi na operesheni za kijeshi na maswala mengine ambayo viongozi wa jeshi la uhifadhi wanapaswa kuyaelewa na kuyafanyia kazi.

“Asilimia 98.6 ya watumishi wa TFS wameshapata mafunzo ya kijeshi hivyo utendaji kwa mfumo wa kijeshi wenye weledi unalenga kuiwezesha taasisi kutekeleza wajibu wake vizuri kukidhi mahitaji na matarajio ya taifa katika uhifadhi wa Misitu na Rasilimali Nyuki ambazo ni kusimamia misitu yote 463 ya hifadhi ya Serikali kuu, mashamba ya miti 24, Hifadhi za misitu ya mazingira asilia 20, misitu ya mikoko katika mwambao wa bahari ya Hindi na misitu iliyo katika ardhi ya jumla.” Anaema Prof. Silayo.


Hata hivyo, Prof. Silayo anasema pamoja na juhudi mbalimbali zinazochukuliwa na TFS kuhifadhi rasilimali hizo bado wanakumbana na changamoto mbalimbali zinazohitaji mbinu mpya za kijeshi za utatuzi wake ambapo kusema mafunzo hayo ni moja ja silaha muhimu kwenye kuongoza mapambano.

Awali Akisoma taarifa fupi ya kuhitimisha mafunzo ya uongozi kwa maofisa hao katika Chuo cha Misitu Cha Olmotonyi, Naibu Kamishna wa Uhifadhi (TFS) anayesimamia Huduma Saidizi, Emmanuel Wilfed alisema mafunzo hayo yalishirikisha maofisa hao 47 na yalianza Januari 9 mwaka huu na kumalizia j Januari 18 mwaka huu.