UUZAJI WA MITI YA MISAJI KWA NJIA YA MNADA WA KIELEKTRONIKI

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) utauza miti aina ya misaji yenye jumla ya  meta za ujazo 10,437.616 iliyopo katika Shamba la miti Mtibwa, Turiani Mkoani Morogoro    na Shamba la miti Longuza, Muheza Mkoani Tanga. Jumla ya meta za ujazo 4,385.087 na 6,052.529 zitauzwa katika shamba la miti Mtibwa na Longuza mtawalia.

Miti itauzwa kwa njia ya mnada wa kielektroniki kwa kuzingatia Kanuni ya 31 (ii) ya Kanuni za Misitu za Mwaka 2004. Mnada huu utafanyika siku ya Jumanne tarehe 2 Agosti, 2022 kwa Shamba la Miti Mtibwa na Jumatano tarehe 3 Agosti, 2022 kwa Shamba la Miti Longuza. Muda wa kuanza mnada itakuwa saa moja kamili (01:00) asubuhi hadi saa kumi kamili (10:00) jioni.

Ili kushiriki kwenye mnada, mshiriki atatakiwa kujisajili kupitia anuani ifuatayo http://mis.tfs.go.tz/e-auction kuanzia tarehe ya tangazo hili hadi saa sita kamili (6:00) usiku wa tarehe 30 Julai, 2022 siku ya Jumamosi. Kwa ajili ya msaada wa usajili, wasiliana na: +255 713 335 926 or +255 766 857 062.

Washiriki wanakaribishwa kukagua miti iliyopo shambani wakati wa saa za kazi kuanzia saa tatu (3:00) asubuhi hadi saa tisa (9:00) alasiri siku za Jumatatu hadi Ijumaa isipokuwa siku za sikukuu. Ukaguzi huo utafanyika kuanzia tarehe ya Tangazo hili hadi tarehe 29 Julai, 2022 siku ya Ijumaa. Mhifadhi Mkuu wa Shamba husika au wasaidizi          wake watakuwepo kwa ajili ya kutoa maelezo ya ziada.

ZAIDI SOMA KIAMBATANISHI

Downloads File: