Habari » News and Events

Mamia wafurika Banda la Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Maonesho ya Saba Saba ya 43

MAMIA ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam na viunga vyake (pichani juu), wamefurika kwenye banda la TFS kwenye maonesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es

Salaam yanayoandaliwa na Mamlaka ya Undelezaji biashara nchini (Tan Trade) kwenye viwanja vya Julius Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Wengi wa wananchi hao ni pamoja na wadau wa misitu na nyuki, wafanyakazi wa umma na binafsi ambao walifika kupata huduma mbalimbali lakini kubwa iliyovutia wengi kuuliza namna wanavyoweza kushiriki safari ya utalii ya Hifadhi ya Magamba.

Akiuliza swali mmoja wa wananchi waliofika bandani hapo Elizabeth Zaya anasema ameona wasanii kama Lina na Amini, Baba yake Diamond na Baby Madah wakiwa Magamba wakifurahia maisha na kutaka kujua anawezaje naye kufika.

Akijibu maswali ya waliohitaji kushiriki safari ya kwenda kutalii katika hifadhi ya mazingira asilia magamba iliyopo wilayani Lushoto mkoani Tanga, Afisa Masoko, Bw. Reubern Nyambita alisema mwananchi anaweza kufika katika banda la TFS lililopo ndani ya banda la Wizara ya Maliasili na Utalii au kupiga simu namba 0757 399 402.

Alisema hifadhi hiyo imesheheni vivutio mbalimbali vya utalii ikiwemo mimea na miti ikiwamo ambayo ni adimu na pia inayopatikana katika eneo hilo pekee, view point itakayokuwezesha kuona taswira ya miji ya lushoto, mombo na korogwe, kivutio cha kipekee, jiwe la mungu na skyline ya pekee Afrika Mashariki nzima iliyotumika kusafirisha magogo kutoka Lushoto hadi Korogwe (20km) kwa dakika 7.

 Nyambita anasema safari hio itafanyika tarehe 12 hadi 14 /06/2019 na zitaanzia katika viwanja vya maonesho ya kibiashara (sabasaba) jijini dar es salaam na kumalizikia hapo hapo.