MABADILIKO YA TAREHE ZA KUUZA WA MITI YA MISAJI KWA NJIA YA MNADA KATIKA SHAMBA LA MITI MTIBWA NA LO

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) utauza miti aina ya misaji yenye jumla ya meta za ujazo 11,270.847 iliyopo katika mashamba ya miti Mtibwa Mkoani Morogoro na Longuza Mkoani Tanga. Jumla ya meta za ujazo 7,062.230 na 4,208.613 zitauzwa katika shamba la miti Mtibwa na Longuza mtawalia.

Miti hiyo iliyokuwa iuzwe tarehe 29 Machi, 2021 katika Shamba la Miti Mtibwa na tarehe 31 Machi, 2021 katika Shamba la Miti Longuza; sasa miti hiyo itauzwa kwa minada ya hadhara katika:

Shamba la Miti Mtibwa siku ya Ijumaa ya tarehe 9 Aprili, 2021 saa 4:30 asubuhi na Shamba la Miti Longuza siku ya Jumatatu ya tarehe 12 Aprili, 2021 saa 4:30 asubuhi.

Maelezo zaidi fungua kiambatanishi chini:-

Pakua Faili: