Habari » News and Events

Kamishna Mhifadhi Misitu Prof. Dos Santos Silayo afanya mazungumzo na wajumbe kutoka EUMETSAT

Kamishna Mhifadhi Misitu Prof. Dos Santos Silayo amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe  kutoka Taasisi ya Umoja wa Ulaya inayorusha picha za matukio na viashiria vya moto kwenye satalaiti  “European Meteorological Satellite Agency (EUMETSAT) uliokuwa unaongozwa na Afisa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Vincent Gabaguo (mwenye miwani).

Pamoja na mambo mengine Prof. Silayo aliwashukuru wajumbe hao kwa kuweza kutoa taarifa za vishiria vya moto kwa njia ya satalaiti na kuiwezesha TFS kupambana na majanga ya moto si kwenye misitu pekee inayoisimamia bali hata kwenye maeneo mengine ya nchi.

“Tuna kitengo kinachoshughulikia moto, monitoring inafanyika muda wote na taarifa husambazwa haraka iwezekanavyo kwa wahusika wa eneo ambalo kuna moto ili waweze kuuzima kabla ya kuleta maafa makubwa,” alisema Prof Silayo.

Wengine walioshiriki mkutano huo ni pamoja na Misimamizi wa Masuala ya Moto wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Kekilia Kabalimu pamoja na afisa wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini, kwenye jengo la Mpingo Jijini Dar es Salaam, leo Agosti 30.