1. Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) unatarajia kuuza miti aina ya Misaji yenye jumla ya meta za ujazo 10,733.56 iliyopo mashamba ya miti ya Mtibwa na Longuza mkoani Morogoro na Tanga mtawalia. Jumla ya meta za ujazo 7,898.82 na 2,834.74 zitauzwa katika shamba la miti Mtibwa na Longuza mtawalia. Miti hiyo iliyopimwa katika vitalu vyenye ujazo mdogo vitauzwa kwa mnada kwa kuzingatia kanuni ya 31 (ii) ya kanuni za Sheria ya Misitu za mwaka 2004. Miti hii ya Misaji itauzwa mahali ilipo na jinsi ilivyo na mnunuzi hatakuwa na haki ya kudai fidia baada ya mauzo.
2. Kampuni au mtu binafsi anayetaka kushiriki mauzo kwa njia ya mnada anatakiwa kuwasilisha maombi (Rejea sehemu ya 14 ya Tangazo) kwenye bahasha iliyofungwa kuonesha nia ya kushiriki mauzo kwa njia ya mnada akiambatisha leseni ya biashara, usajili wa kiwanda cha kuchakata magogo (2019/2020) au mkataba, Usajili wa biashara ya mazao ya misitu (2019/2020) na cheti cha utambulisho wa mlipa kodi (TIN). Aidha, anatakiwa aoneshe jina la shamba, namba ya kitalu/vitalu na ujazo anaotarajia kununua kama ilivyo kwenye jedwali namba 1 na 2 hapo chini.
3. Mnada utaendeshwa hadharani wakiwepo wanunuzi wote katika ofisi za mashamba husika. Mnada katika shamba la miti Mtibwa utafanyika siku ya Jumatatu tarehe 27 Aprili, 2020 saa 4:30 asubuhi na katika shamba la miti Longuza mnada utafanyika siku ya Jumatano tarehe 29 Aprili, 2020 saa 4:30 asubuhi. Mnada utafanyika kwa kufuata Sheria ya Misitu Sura 323.
4. Kila kitalu kitanadiwa peke yake kulingana na bei na ujazo uliopo. Hata hivyo, bei ya juu iliyotolewa na mnunuzi wakati wa kufungua bahasha haitazuia wanunuzi wengine kuongeza bei zaidi ya iliyotajwa awali.
5. Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania unawaalika wanunuzi kununua miti ya misaji kwa njia ya mnada ambapo mnunuzi anaweza kuchagua mojawapo kati ya vitalu vifuatavyo: -
Na. |
Jina la Kitalu |
Ujazo kwa Kitalu (m3) |
Bei ya kuanzia kwa kila meta za ujazo (TZS/M3) |
1 |
LG8 - 22 |
261.85 |
630,000 |
2 |
KS12 - A11 |
387.95 |
720,000 |
3 |
KS12 - A12 |
343.09 |
720,000 |
4 |
KS12 - A13 |
387.95 |
720,000 |
5 |
KS12 - A15 |
299.23 |
720,000 |
6 |
KH10 - 10 |
515.37 |
720,000 |
7 |
KS12 - A19 |
158.94 |
720,000 |
8 |
KS12 - A22 |
153.30 |
720,000 |
9 |
KS12 - A24 |
171.49 |
720,000 |
10 |
KS12 - A30 |
155.57 |
720,000 |
JUMLA |
2,834.74 |
|
JEDWALI Na.1:ORODHA YA VITALU, UJAZO NA BEI KWA SHAMBA LA MITI LONGUZA
JEDWALI Na.2: ORODHA YA VITALU, UJAZO NA BEI KWA SHAMBA LA MITI MTIBWA
Jina la Kitalu |
Ujazo kwa kitalu (M3) |
Bei ya kuanzia kwa kila meta za ujazo (TZS/M3) |
|
1 |
LR 12A |
307.57 |
260,000 |
2 |
LR 12A-1 |
205.76 |
340,000 |
3 |
LR 12A-2 |
229.57 |
260,000 |
4 |
LR 12A-3 |
207.14 |
260,000 |
5 |
LR 12A-4 |
217.96 |
260,000 |
6 |
LR 12A-5 |
144.05 |
360,000 |
7 |
LR 12A-6 |
218.68 |
230,000 |
8 |
LR 12A-7 |
242.85 |
250,000 |
9 |
LR 12A-8 |
210.30 |
190,000 |
10 |
LR 12A-9 |
235.37 |
180,000 |
11 |
LR 12A-10 |
201.30 |
190,000 |
12 |
LR 12A-11 |
303.98 |
200,000 |
13 |
LR 12A-12 |
103.38 |
240,000 |
14 |
LR 12A-13 |
204.31 |
210,000 |
15 |
LR 12A-14 |
115.95 |
240,000 |
16 |
LR 12A-15 |
193.56 |
270,000 |
17 |
FN 64-16 |
167.67 |
280,000 |
18 |
FN 64-17 |
226.59 |
310,000 |
19 |
LR 16B-18 |
303.39 |
330,000 |
20 |
LR 16B-20 |
400.31 |
370,000 |
21 |
LR 16B-23 |
342.44 |
310,000 |
22 |
LR 16B-24 |
129.10 |
330,000 |
23 |
LR 16B-25 |
147.03 |
300,000 |
24 |
LR 16B-26 |
326.09 |
260,000 |
25 |
LR 16B-27 |
300.19 |
210,000 |
26 |
LR 16B-28 |
230.37 |
220,000 |
27 |
LR 16B-29 |
190.49 |
240,000 |
28 |
LR 16B-30 |
178.43 |
180,000 |
29 |
LR 16B-31 |
140.20 |
330,000 |
30 |
LR 16B-32 |
198.38 |
280,000 |
31 |
LR 14-33 |
57.04 |
230,000 |
32 |
LR 14-34 |
69.12 |
180,000 |
33 |
LR 14-35 |
69.12 |
200,000 |
34 |
LR 14-36 |
92.38 |
210,000 |
35 |
LR 14-37 |
132.22 |
190,000 |
36 |
LR 14-38 |
137.56 |
210,000 |
37 |
LR 14-39 |
158.65 |
210,000 |
38 |
LR 14-40 |
231.64 |
200,000 |
39 |
LR 14-41 |
173.43 |
170,000 |
40 |
LR 14-42 |
155.26 |
130,000 |
JUMLA |
7,898.82 |
|
6. Hati ya ushindi kwa mnunuzi aliyetaja kiwango cha juu kwa kila kitalu wakati wa mnada itatolewa.
7. Mnunuzi atakayefanikiwa kununua miti ya misaji hataruhusiwa kusafirisha magogo nje ya nchi kwa mujibu wa kanuni ya 50(1) ya kanuni za misitu za mwaka 2004.
8. Makampuni na watu binafsi wanakaribishwa kutembelea vitalu shambani wakati wa saa za kazi kuanzia saa tatu (3:00) asubuhi hadi saa tisa (9:00) alasiri isipokuwa siku za sikukuu. Meneja wa shamba au msaidizi wake atakuwepo kwa ajili ya maelekezo zaidi.
9. Wanunuzi wanapaswa kuchukua na kusoma masharti ya uvunaji kwa kila shamba. Masharti hayo yanapatikana ofisi za shamba husika.
10. Bei ya kianzio kwa mita moja ya ujazo imeoneshwa katika Jedwali namba 1 na 2 hapo juu ikijumuisha ‘VAT’, ‘CESS’ na ‘LMDA’.
- Mnunuzi atakayeshinda atalipa asilimia ishirini na tano (25%) ya thamani yote ya ununuzi ndani ya siku tatu (3) baada ya mnada kufanyika. Fedha hizo hazitarudishwa. Asilimia sabini na tano (75%) iliyobaki italipwa ndani ya siku kumi na nne (14) baada ya mnada. Malipo yote yafanyike kwa kupitia mfumo wa makusanyo ya Serikali (GePG) baada ya kupewa Hati ya madai (Bill) ya mfumo kupitia Bank ya NMB, CRDB, Tigo au M-Pesa. Hati ya madai inayoonesha kiasi cha kulipa itatolewa na Meneja wa shamba husika.
- Mnunuzi atapaswa kuwasilisha hati ya malipo kwa meneja wa shamba husika kama uthibitisho wa malipo si zaidi ya siku tatu (3) baada ya malipo kufanyika.
- Mteja atatakiwa kuondoa mazao ya misitu aliyonunua ndani ya miezi miwili (siku sitini) baada ya kumaliza kulipa malipo yote kwa asilimia 100.
- Maombi yote yawasilishwe siku ya mauzo kabla ya saa 4:00 asubuhi. Aidha, wanunuzi watakaochelewa kuwasilisha maombi yao kwa siku na muda uliopangwa hawataruhusiwa kushiriki katika mnada.
- Tangazo hili pia linapatikana katika tovuti zifuatazo za Wakala na Wizara: www.tfs.go.tz na www.mnrt.go.tz
ANGALIZO
Mshiriki atakayeshinda na kupewa hati ya ushindi na kisha yeye mwenyewe kushindwa kulipia mgawo huo ndani ya muda aliopewa (kadiri inavyoelezwa katika kipengele 11 cha tangazo hili) kwa sababu yoyote ile, atakuwa ametenda kosa la kuhujumu mnada na kwa makusudi kuikosesha Serikali mapato hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake ikiwemo kudaiwa fidia ya hasara itakayosababishwa na kitendo hicho chini ya Sheria ya Makosa ya Uhujumu Uchumi (Sura ya 200 marejeo ya 2002).
limetolewa na
KAMISHNA WA UHIFADHI
S.L.P 40832,
DAR ES SALAAM
13.04.2020
TANGAZO LA UUZAJ I WA MAZAO YA MISITU YALIYOPO KATIKA KITUO MENEJA WA MISITU WILAYA YA TANGA NA MAZAO YA MISITU YALIYOPO KATIKA KITUO MENEJA WA MISITU WILAYA YA TANGA