Habari »

MABADILIKO YA TAREHE YA KUUZA MAGOGO YA MKURUNGU KWA NJIA YA MNADA KATIKA BANDARI YA NCHI KAVU

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) utauza magogo vipande 18,489 ya mti wa Mkurungu (Pterocarpus Tinctorius) yenye jumla ya meta za ujazo 1,357.026 iliyopo katika eneo la Bandari ya Nchi Kavu – Ubungo, Dar es Salaam.

Magogo hayo yaliyokuwa yauzwe tarehe 29 Machi, 2021 katika eneo la Bandari ya Nchi Kavu – Ubungo, sasa yatauzwa kwa mnada wa hadhara katika eneo la Bandari ya Nchi Kavu – Ubungo siku ya Alhamisi ya tarehe 08 Aprili, 2021 kuanzia saa 4:30 asubuhi.

Magogo hayo ya Mkurungu yamepimwa ujazo uliopo katika makasha  59 na yatauzwa kwa njia ya mnada kwa kuzingatia Kanuni ya 31 (ii) ya Kanuni za Sheria ya Misitu za Mwaka 2004. Magogo hayo yatauzwa mahali yalipohifadhiwa na jinsi yalivyo na mnunuzi hatakuwa na haki ya kudai fidia baada ya mauzo.

Mnunuzi anakaribishwa kutembelea eneo la Bandari ya Nchi Kavu - Ubungo ili kukagua mazao hayo ya misitu katika muda wa kazi kuanzia saa tatu (3:00) asubuhi hadi saa tisa (9:00) alasiri siku za Jumatatu hadi Ijumaa isipokuwa siku za sikukuu. Aidha, Maafisa Misitu wa Wakala watakuwepo katika Bandari ya Nchi Kavu - Ubungo kwa ajili ya kutoa maelezo ya ziada ikiwa yatahitajika. 

Mnunuzi mwenye nia ya kushiriki mnada anatakiwa kuwasilisha kwenye bahasha iliyofungwa nia yake ya kushiriki mauzo kwa njia ya mnada akiainisha namba ya kasha na pendekezo la bei kwa meta moja ya ujazo anaotarajia kununua kwa kufuata orodha kwenye Jedwali namba 1 la Tangazo hili. Aidha, Jedwali hili litatumika kuchagua kasha lenye magogo ya kununua kwa kuzingatia taarifa zilizoorodheshwa kama ifuatavyo (fungua kimbatanishi chini):-

Pakua Faili: