Kuhusu Wakala

Karibu

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ((Tanzania Forest Services (TFS) Agency)) ulianzishwa kisheria kupitia Tangazo la Gazeti la Serikali (GN 269) la tarehe 30/7/2010 na kuzinduliwa rasmi tarehe 18/7/2011.

Lengo Kuu la Kuanzishwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Kwa kuzingatia programu tajwa, Wakala wa Huduma za Misitu umeundwa kwa madhumuni ya kuhakikisha: Uwepo wa usimamizi madhubuti na wenye ufanisi na tija wa rasilimali za misitu na nyuki; kuongeza ubora na thamani ya kifedha katika kutoa huduma kwa umma; na kuendelea kukuza na kuboresha uwezo wa kutoa huduma kwa umma.

Katika muktadha huu, masuala ya uendelezaji sera na sheria, pamoja na kanuni na taratibu zake yanashughuliwa na Idara ya Misitu na Nyuki katika Wizara ya Maliasili na Utalii. Hata hivyo majukumu ya Wakala yameongezeka licha ya kutoshughulikia sera na sheria. Wakala umepanua wigo kibiashara na kuongeza maeneo ya uzalishaji miti na mazao ya nyuki ili kukidhi mahitaji halisi, shughuli za uwekezaji, kuboresha njia mbadala za mapato na uboreshaji wa hifadhi za misitu na nyuki kwa ujumla.