Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) utauza miti aina ya misaji yenye jumla ya meta za ujazo 6,755.935 iliyopo katika mashamba ya miti Mtibwa Mkoani Morogoro na Longuza Mkoani Tanga. Jumla ya meta za ujazo 3,022.410 na 3,733.525 zitauzwa katika shamba la miti Mtibwa na Longuza mtawalia. Miti hiyo iliyopimwa ujazo katika viunga itauzwa kwa mnada kwa kuzingatia Kanuni ya 31 (ii) ya Kanuni za Sheria ya Misitu za Mwaka 2004.