Resources » News and Events

UUZAJI WA MITI YA MISAJI KWA NJIA YA MINADA YA HADHARA KATIKA MASHAMBA YA MITI YA MTIBWA NA LONGUZA

MMOJA WA WANUNUZI WA TEAK AKIPIMA GOGO LA MTI ALIOVUNA KUTOKA KWENYE SHAMBA LA MTIBWA

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) utauza miti aina ya misaji yenye jumla ya meta za ujazo 8,676.111 iliyopo katika mashamba ya miti Mtibwa Mkoani Morogoro na Longuza Mkoani Tanga. Jumla ya meta za ujazo3,428.629 na 5,247.482 zitauzwa katika shamba la miti Mtibwa na Longuza mtawalia.

Miti imepimwa ujazo katika viunga vya mashamba ya Mtibwa na Longuza itauzwa kwa njia ya minada kwa kuzingatia Kanuni ya 31 (ii) ya Kanuni za Sheria ya Misitu za Mwaka 2004. Miti hiyo ya misaji itauzwa mahali ilipo na jinsi ilivyo na mnunuzi hatakuwa na haki ya kudai fidia baada ya mauzo.

Minada ya hadhara itafanyika katika ofisi za Shamba la Miti Mtibwa siku ya Jumanne ya tarehe 17 Agosti, 2021 saa 4:30 asubuhi na Shamba la Miti Longuza siku ya Alhamisi ya tarehe 19 Agosti, 2021 saa 4:30 asubuhi.

Wanunuzi wanakaribishwa kukagua mali iliyopo shambani wakati wa saa za kazi kuanzia saa tatu (3:00) asubuhi hadi saa tisa (9:00) alasiri siku za Jumatatu hadi Ijumaa isipokuwa siku za sikukuu. Mhifadhi Mkuu wa Shamba husika au wasaidizi wake watakuwepo kwa ajili ya kutoa maelezo ya ziada.

Mnunuzi mwenye nia ya kushiriki mnada anatakiwa kuwasilisha kwenye bahasha iliyofungwa nia yake ya kushiriki mauzo kwa njia ya mnada akiainisha jina la shamba, namba ya kitalu (ploti) na pendekezo la bei kwa kila meta ya ujazo anaotarajia kununua kwa kufuata orodha kwenye Jedwali namba 1 na Jedwali namba 2 la Tangazo hili.

Uchaguzi wa vitalu vya kununua unaweza kufanyika kwa kuzingatia taarifa zilizoorodheshwa katika Jedwali namba 1 na Jedwali namba 2 kama ilivyoonyeshwa kwenye PDF file 

Downloads File: