Resources » News and Events

UUZAJI WA MAGOGO YA MTI WA MKURUNGU KWA NJIA YA MNADA KATIKA ENEO LA BANDARI YA NCHI KAVU – UBUNGO,

PICHANI NI MAGOGO YA MTI AINA YA MISAJI HAYANA UHUSIANO NA MAGOGO YANAYOKWENDA KUUZWAPICHANI NI MAGOGO YA MTI AINA YA MISAJI HAYANA UHUSIANO NA MAGOGO YANAYOKWENDA KUUZWA

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) utauza magogo vipande 18,489 ya mti wa Mkurungu (Pterocarpus Tinctorius) yenye jumla ya meta za ujazo 1,357.026 iliyopo katika eneo la Bandari ya Nchi Kavu – Ubungo, Dar es Salaam. Magogo hayo yaliyopimwa ujazo katika makontena 59 yatauzwa kwa mnada kwa kuzingatia Kanuni ya 31 (ii) ya Kanuni za Sheria ya Misitu za Mwaka 2004. Magogo hayo ya Mkurungu yatauzwa mahali yalipohifadhiwa na jinsi yalivyo na mnunuzi hatakuwa na haki ya kudai fidia baada ya mauzo.

Mnada utaendeshwa hadharani wakiwepo wanunuzi wote katika eneo laBandari ya Nchi Kavu - Ubungo. Mnada utafanyika siku ya Jumatatu ya tarehe 29 Machi, 2021 saa 4:30 asubuhi.

Mnunuzi anakaribishwa kutembelea eneo la Bandari ya Nchi Kavu - Ubungo ili kukagua mazao hayo ya misitu muda wa kazi kuanzia saa tatu (3:00) asubuhi hadi saa tisa (9:00) alasiri siku za Jumatatu hadi Ijumaa isipokuwa siku za sikukuu. Ukaguzi huo utafanyika kuanzia tarehe ya Tangazo hili hadi tarehe 28 Machi, 2021. Aidha, Maafisa Misitu wa Wakala watakuwepo kwa ajili ya kutoa maelezo ya ziada ikiwa yatahitajika.

Mnunuzi mwenye nia ya kushiriki mnada anatakiwa kuwasilisha kwenye bahasha iliyofungwa nia ya kushiriki mauzo kwa njia ya mnada akiainisha namba ya kontena na pendekezo la bei kwa meta moja ya ujazo anaotarajia kununua kwa kufuata orodha kwenye Jedwali namba 1 la Tangazo hili (fungua kiambatanishi kwa taarifa zaidi). 

UUZAJI WA MITI YA MISAJI KWA NJIA YA MNADA KATIKA SHAMBA LA MITI MTIBWA NA LONGUZA (TAZAMA KIAMBATANISHI)

THE SALE OF STANDING TEAK TREES BY AUCTION AT MTIBWA AND LONGUZA FOREST PLANTATIONS ( DETALS ATTACHED)

Downloads File: