Resources » News and Events

TANGAZO LA MNADA WA MKURUNGU MKOANI TABORA 20 SEPTEMBA, 2021

UUZAJI WA MAGOGO YA MTI AINA YA MKURUNGU KWA NJIA YA MNADA KATIKA KIJIJI CHA WACHAWASEME (IGAGALA No 9) NA KIJIJI CHA MPWAGA (IGAGALA No3) WILAYANI KALIUA MKOA WA TABORA 

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) utauza magogo ya Mkurungu (Pterocarpus tinctorius) jumla ya vipande 7,456 vyenye jumla ya meta za ujazo 1,758.793. Magogo haya yapo katika Kijiji cha Wachawaseme na Mpwaga, Tarafa ya Igagala, wilaya ya Kaliua, Mkoani Tabora. 

Magogo hayo ya Mkurungu yamepimwa na yamepangwa katika mafungu (Lots) 10 na yatauzwa kwa njia ya mnada wa hadhara kwa kuzingatia Kanuni ya 31 (ii) ya Kanuni za Sheria ya Misitu za Mwaka 2004. Magogo hayo yatauzwa mahali yalipohifadhiwa na jinsi yalivyo na mnunuzi hatakuwa na haki ya kudai fidia baada ya mauzo. 

Mnada utafanyika hadharani katika vijiji vya Wachawaseme na Mpwaga wakiwepo wanunuzi wote. Mnada utafanyika siku ya Jumatatu ya tarehe 20 Septemba, 2021 kuanzia saa 4:30 asubuhi. 

Mnunuzi anakaribishwa kutembelea Kijiji cha Wachawaseme na Mpwaga kulipopangwa mafungu (loti) ya Magogo ya Mkurungu ili kukagua mazao hayo ya misitu muda wa kazi kuanzia saa tatu (3:00) asubuhi hadi saa tisa (9:00) alasiri siku za Jumatatu hadi Ijumaa. Ukaguzi huo utafanyika kuanzia tarehe ya Tangazo hili hadi tarehe 19 Septemba, 2021. Aidha, Maafisa Misitu wa TFS watakuwepo kwa ajili ya kutoa maelezo ya ziada ikiwa yatahitajika. Unaweza kuona jedwali kwenye PDF iliyoambatanishwa hapa ili kuchagua fungu lenye magogo ya kununua kwa kuzingatia taarifa zilizoorodheshwa.

Downloads File: