Resources » News and Events

Mnada wa uuzaji wa Miti ya Misaji, Korogwe na Longuza

 Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) unatarajia kuuza miti aina ya misaji yenye jumla ya meta za ujazo 8,113.177 iliyopo katika shamba ya miti Mtibwa mkoani Morogoro na Longuza mkoani Tanga. Jumla ya meta za ujazo 4,017.02 na 4,096.157 zitauzwa katika shamba la miti Mtibwa na Longuza mtawalia. Miti hiyo iliyopimwa ujazo katika viunga itauzwa kwa mnada kwa kuzingatia Kanuni ya 31 (ii) ya Kanuni za Sheria ya Misitu za Mwaka 2004. Miti hiyo ya misaji itauzwa mahali ilipo na jinsi ilivyo na mnunuzi hatakuwa na haki ya kudai fidia baada ya mauzo.

Mnada utaendeshwa hadharani wakiwepo wanunuzi wote katika ofisi za shamba husika. Mnada katika Shamba la Miti Mtibwa utafanyika siku ya Jumatatu tarehe 23 Novemba, 2020 saa 4:30 asubuhi na katika Shamba la Miti Longuza, mnada utafanyika siku ya Jumatano tarehe 25 Novemba, 2020 saa 4:30 asubuhi.

Downloads File: