Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) unatarajia kuuza miti aina ya Misaji yenye jumla ya meta za ujazo 1,600.883 iliyopo katika mipaka ya Misitu ya Hifadhi ya Kwani na Tongwe Wilayani Muheza na Msitu wa Hifadhi ya Mazingira Asilia Nilo wilayani Korogwe. Jumla ya meta za ujazo 631.20, 602.89 na 366.703 zitauzwa katika Msitu wa hifadhi wa Tongwe, Kwani na Nilo. Miti hiyo itauzwa kwa mnada kwa kuzingatia kanuni ya 31 (ii) ya kanuni za Sheria ya Misitu za mwaka 2004. Miti hii ya Misaji itauzwa mahali ilipo na jinsi ilivyo na mnunuzi hatakuwa na haki ya kudai fidia baada ya mauzo.