Resources » News and Events

Mnada wa Miti ya Misaji

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) unatarajia kuuza miti aina ya Misaji yenye jumla ya meta za ujazo 9,452.74 iliyopo mashamba ya miti ya Mtibwa na Longuza mkoani Morogoro na Tanga mtawalia. Jumla ya meta za ujazo 6,618.00 na 2,834.74 zitauzwa katika shamba la miti Mtibwa na Longuza mtawalia. Miti hiyo iliyopimwa katika ploti zenye ujazo mdogo zitauzwa kwa mnada kwa kuzingatia kanuni ya 31 (ii) ya kanuni za Sheria ya Misitu za mwaka 2004. Miti hii ya Misaji itauzwa mahali ilipo na jinsi ilivyo na mnunuzi hatakuwa na haki ya kudai fidia baada ya mauzo.

Downloads File: