Resources » News and Events

MNADA WA KUUZA MITI YA MISINDANO KATIKA SHAMBA LA MITI LA SAO HILL

MNADA WA KUUZA MITI YA MISINDANO (Pinus Spp) KATIKA VITALU VILIYOATHIRIWA NA MOTO KATIKA SHAMBA LA MITI LA SAO HILL- TARAFA YA KWANZA WILAYANI MUFINDI

 

 

TAREHE YA MNADA       :    25 MACHI,2020

TAREHE YA TANGAZO   :    12 MACHI,2020

MAHALI:  UKUMBI WA MIKUTANO ULIOPO MAKAO MAKUU YA SHAMBA (SAO HILL SOCIAL HALL); MTAA WA IHEFU-MAFINGA

MUDA:  SAA NNE KAMILI ASUBUHI (10:00HRS)

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)-Shamba la Miti Sao Hill unatarajia kuuza kwa njia ya mnada wa hadhara miti aina ya Misindano yenye jumla ya meta za ujazo 9,252.02 ambazo zimo katika vitalu ambavyo vilipata athari ya Moto katika tarafa ya Kwanza-Irundi

 Uuzaji huo kwa njia ya mnada (Auction) unafanyika kwa kuzingatia kanuni ya 31 kifungu cha (ii) cha kanuni za Misitu za mwaka 2004. Mnada utafanyika tarehe 25 Machi, 2020 katika ukumbi wa mikutano wa Shamba (Sao Hill Social Hall) uliopo Makao Makuu ya Ofisi za Shamba la Miti Sao Hill -Ihefu kuanzia Saa nne kamili (4.00) asubuhi. Miti itauzwa kwa mafungu (LOTS) mahali ilipo na jinsi ilivyo kama inavyooneshwa katika jedwali la mchanganuo la tangazo hili na mnunuzi hatakuwa na haki ya kudai fidia ya ujazo baada ya mauzo.

Masharti ya Mnada

  1. Kampuni au Mtu binafsi mwenye nia ya kushiriki ununuzi wa miti hii ya Misindano kwa njia ya mnada anatakiwa kufika kwenye mnada kwa wakati sahihi akiwa na usajili wa biashara ya Mazao ya Misitu wa mwaka 2019/2020, cheti cha utambulisho wa mlipa kodi (TIN) na Leseni ya biashara
  2. Mnunuzi atalipa asilimia ishirini na tano (25%) ya thamani yote ya ununuzi wa ujazo alioshinda siku ya mnada. Fedha hizo hazitarudishwa endapo mhusika atashindwa kukamilisha asilimia 75% iliyobaki ndani ya siku kumi na nne (14). Asilimia sabini na tano (75%) iliyobaki italipwa ndani ya siku kumi na nne (14) baada ya mnada .Malipo yote yafanyike kwa kupitia mfumo wa makusanyo ya serikali (GePG) baada ya kupewa Hati ya Madai (Bill) ya mfumo kupitia Bank ya CRDB,NMB, Tigo Pesa, au Mpesa. Hati ya madai inayoonesha kiasi cha kulipa itatolewa na Mhifadhi wa Shamba la miti Sao Hill.
  3. Mnunuzi atapaswa kuwasilisha hati ya malipo kwa Mhifadhi Mkuu wa  Shamba la Miti la Sao Hill kama uthibitisho wa malipo siyo zaidi ya siku tatu (3) baada ya malipo kufanyika
  4. Mnunuzi/Wanunuzi watakaoshinda watapewa leseni ya kuvuna miti ya misindano na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ndani ya siku saba baada ya kukamilisha malipo ya gharama zote kwa asilimia 100%.
  5. Mnunuzi atakayefanikiwa kununua miti ya misindano hataruhusiwa kusafirisha magogo nje ya nchi isipokuwa baada ya kuchakata kwa mujibu wa kifungu cha 50 (1) cha kanuni za misitu za mwaka 2004 na Tangazo la Serikali Na.69 la Mwaka 2006.
  6. Mnada utaendeshwa hadharani  tarehe 25 Machi,2020 kwa kufuata sheria ya Misitu Sura 323. Wanunuzi wote wenye nia ya kushiriki mnada wafike eneo la Ihefu katika ukumbi wa Mikutano (Social Hall) zilipo ofisi za Makao Makuu ya Shamba la Miti la Sao Hill. Aidha miti iliyoathiriwa na moto itanadiwa kwa mafungu (LOTS) kama ilivyoainishwa katika jedwali la tangazo hili.
  7. Mnunuzi atatangazwa kuwa Mshindi wa fungu (LOT) husika pale tu atakapokuwa amewashinda washindani wake wote na amefikia au kuzidi bei elekezi (Reserve price) iliyowekwa na serikali na kukabidhiwa mnadishaji siku ya mnada kwa ajili ya rejea
  8. Mnunuzi mwenye nia ya kununua kiunga husika atataja bei yake (offer); lakini mnadishaji katika mnada atazingatia sharti namba saba (7) la tangazo hili katika kumtangaza mshindi.
  9. Makampuni na watu binafsi wanakaribishwa kutembelea vitalu na viunga vilivyoainishwa katika jedwali la tangazo wakati wa saa za kazi kuanzia saa mbili (2.00) asubuhi hadi saa tisa na nusu (9.30) alasiri isipokuwa siku za sikukuu na mapumziko ya mwisho wa Juma. Meneja wa tarafa ya kwanza atahusika kusimamia jukumu hili
  10.  Bei  ya mauzo katika mnada itajumuisha (VAT), (CESS), TaFF na Forest Royalty, LMDA, Hati ya kusafirisha mazao ya Misitu (T.P), na Ada ya Leseni

Imetolewa na:

MHIFADHI MKUU WA SHAMBA LA MITI SAO HILL

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA

S.L.P 45

MAFINGA

 

Kwa yeyote atakayehitaji ufafanuzi juu ya Tangazo hili atumie 

          SIMU NA. +255 674 316 819

                        +255 782 581199

   BARUA PEPE:   saohill@tfs.go.tz

               pmu_saohill@tfs.go.tz

Downloads File: