Resources » News and Events

KATIBU MKUU MALIASILI NA UTALII AHIMIZA WATUMISHI TFS KUWA NA SIKU MAALUMU YA KUKUTANA NJE YA KAZI.

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na utalii Dkt Francis Michael akiwa katika ziara ya kikazi Ofisi ya TFS Makao Makuu Mpingo house jijini Dar es salaam tarehe 29/03/2022, amemhimiza Kamishna wa Uhifadhi TFS Profesa Dos Santos Silayo kuandaa siku maalumu kwa ajiri ya Watumishi kukutana kama familia mazingira ya nje ya kazi.

Dkt Michael amesema kufanya hivyo kutawapa Watumishi hao nafasi ya kuelezea hisia zao kuhusu kazi na majukumu yao.

"kwa hiyo Profesa nafikiri utaandaa hii siku, Watumishi wakutane, iwe tu get together kama TFS day angalau watu wakutane, wafurahie maisha na ninajua mtaniambia kama amewaandalia hii siku" Dkt Michael. 

Katika ziara hiyo Dkt Michael amewataka Watumishi hao kufanya kazi kwa bidii kwa kuzingatia maadili ya Jeshi la Uhifadhi na kujiepusha na vitendo vinavyokiuka maadili ya Jeshi hilo.

"Tuendelee kufanya kazi kwa bidii huku tukitumia zaidi busara, tujiepushe na vitendo vinavyotuchafua, sisi ni Jeshi kwa hiyo mnaonekana zaidi." Dkt Michael. 

Naye Mkurugenzi wa Utawala Wizara ya Maliasili na utalii Bi Prisca Lwangili amewataka watumishi hao kuelewa kuwa kufanya ya Uhifadhi ni kufanya Kazi ya Mungu.

Akizungumza katika kikao hicho Kamishna wa Uhifadhi TFS Profesa Dos Santos Silayo amemkaribisha Katibu Mkuu ambapo ameshukuru kwa kufanya ziara hiyo muhimu na kuahidi kutekeleza yote yaliyoelekezwa katika kikao hicho.