12
Feb
WATAALAM IDARA YA MISITU ZANZIBAR WAWASILI MANYONI KUONGEZA WELEDI SHUGHULI ZA UFUGAJI NYUKI
MANYONI, 12 Februari 2026 — Askari wa Uhifadhi - Ufugaji Nyuki Wilaya ya Manyoni, Jacline Leshabari, akiwasilisha mada kuhusu uanzishaji na usimamizi bora wa hifadhi za nyuki kwa wataalamu kutoka Idara ya Misitu Zanzibar. Mafunzo hayo yamelenga kuimarisha uelewa wa kitaalamu na kubadilishana uzoefu katika kukuza sekta ya ufugaji nyuki.