Habari » News and Events

Uuzaji kwa Njia ya Mnada wa Magogo Yaliyokamatwa na Kutaifishwa Nyanda za Juu Kusini

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) unatarajia kuuza magogo ya miti ambayo yalivunwa kinyume cha sheria ya misitu. Magogo ya Mkulungu (Pterocarpus tinctorius) yana jumla ya meta za ujazo 912.13 na magogo ya Mseni (Brachystegia spp) yana meta za ujazo 31.27.

Magogo yote yapo maeneo mbalimbali ya wilaya katika kanda ya Nyanda za juu kusini. Mauzo haya yatafanyika katika maeneo ambapo magogo yapo kuanzia saa nne na nusu (4:30) asubuhi. Tarehe ya mauzo imeoneshwa katika Jedwali Na.1. Uuzaji huu utafanyika kwa njia ya Mnada (Auction) kwa kuzingatia kanuni 31 (ii) ya kanuni za sheria ya misitu za mwaka 2004. Aidha, magogo yote yatauzwa mahali yalipo na jinsi yalivyo na mnunuzi hatakuwa na haki ya kudai fidia baada ya mauzo.

Pakua Faili: