Uuzaji wa Miti ya Misaji Kwa Njia ya Mnada

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) unatarajia kuuza miti aina ya Misaji yenye jumla ya meta za ujazo 11,395.937 iliyopo katika mashamba ya miti ya Mtibwa na Longuza mkoani Morogoro na Tanga mtawalia. Jumla ya meta za ujazo 5,032.95 na 6,362.987 zitauzwa katika shamba la miti Mtibwa na Longuza mtawalia. Miti hiyo iliyopimwa katika ploti zenye ujazo mdogo zitauzwa kwa mnada tarehe 04 Novemba, 2019 katika shamba la miti Mtibwa na tarehe 06 Novemba, 2019 katika shamba la miti Longuza kwa kuzingatia kanuni ya 31 (ii) ya Kanuni za Sheria ya Misitu za Mwaka 2004. Miti hiyo ya Misaji itauzwa mahali ilipo na jinsi ilivyo na mnunuzi hatakuwa na haki ya kudai fidia baada ya mauzo.

Pakua Faili: