Resources » News and Events

Maombi ya uvunaji msitu kwa 2019/2020

Katika kipindi cha 2019/2020 Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) unategemea kuuza mazao ya misitu (miti/magogo) katika mashamba 11 ya miti ya kupanda.

Wakala unakaribisha maombi ya uvunaji msitu kwa 2019/2020 kutoka kwa Wamiliki wa viwanda vya kuchakata magogo vilivyohakikiwa na kusajiliwa na Wakala. Maombi ya uvunaji msitu yatumwe kwa Meneja wa shamba la Miti husika (rejea jedwali) kuanzia tarehe 27 Mei hadi 12 Juni, 2019 kwa kujazo fomu ya maombi ya uvunaji msitu 2019/2020. Fomu za maombi zinapatikana katika tovuti ya Wakala http://www.tfs.go.tz/index.php/en/resources/category/downloads na ofisi ya meneja wa shamba.

Jedwali Na. 1: Orodha ya mashamba ya miti na jamii ya miti inayopatikana katika mashamba hayo

Na.

Jina la shamba

Anwani

Mahali lilipo

Aina ya miti

1

Sao Hill

S.L.P 45, Mafinga

Mufindi- Iringa

Misindano(Pinus patula)

Mikaratusi (Eucalyptus)

2

Meru/Usa

S.L.P 1257 Arusha

Arumeru- Arusha

Misindano(Pinus patula)

Mikaratusi (Eucalyptus)

Loliondo (Olea capensis)

3

Buhindi

S.L.P 1480 Mwanza

Sengerema- Mwanza

Misindano (Pinus caribaea)

4

North Kilimanjaro (Rongai)

S.L.P 40 Tarakea.

Rombo –Kilimanjaro

Misindano

5

West Kilimanjaro

S.L.P 161 Hai

Hai- Kilimanjaro

Misindano (Pinus patula)

Mikaratusi

6

Shume

S.L.P 60 Lushoto

Lushoto- Tanga

Misindano

7

Kawetire

S.L.P 770 Mbeya

Mbeya

Misindano (Pinus patula)

8

Kiwira

S.L.P 991 Mbeya

Rungwe- Mbeya

Misindano

9

Rubya

S.L.P 134  Nansio

Ukerewe- Mwanza

Misindano

10

Rubare

S.L.P 930 Bukoba

Bukoba- Kagera

Misindano

11

Ukaguru

S.L.P 2 GAIRO

Gairo- Morogoro

Misindano

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Limetolewa na

Mtendaji Mkuu

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania