UUZAJI WA MITI YA TEAK MASHAMBA YA MITI MTIBWA (MOROGORO) NA LONGUZA (TANGA)

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) unatarajia kuuza miti aina ya Misaji yenye jumla ya meta za ujazo 7,067.338 zilizopo katika shamba la miti Mtibwa Mkoani Morogoro na Longuza Mkoani Tanga. Jumla ya meta za ujazo 2,111.516 zinatarajiwa kuuzwa katika shamba la miti Mtibwa na meta za ujazo 4,955.822 katika shamba la miti Longuza. Mauzo haya yatafanyika Mei 10, 2017 katika ofisi za shamba la miti Mtibwa saa nne na nusu (4:30) asubuhi na Mei 12, 2017 katika ofisi za shamba la miti Longuza saa nne na nusu (4:30) asubuhi. Uuzaji huu utafanyika kwa njia ya Mnada (Auction) kwa kuzingatia kanuni 31 (ii) ya Kanuni za Sheria ya Misitu za Mwaka 2004. Miti hii ya Misaji itauzwa mahali ilipo na jinsi ilivyo na mnunuzi hatakuwa na haki ya kudai fidia baada ya mauzo.

PRESS_SWAHILI_May_2017

  • Google+
  • PrintFriendly