Resources » News and Events

Uuzaji wa Miti ya Misaji Shamba la Miti Mtibwa, Morogoro na Longuza, Muheza Tanga

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) unatarajia kuuza miti aina ya Misaji yenye jumla ya meta za ujazo 8,860.74 iliyopo mashamba ya miti ya Mtibwa na Longuza yaliyopo mikoa ya Morogoro na Tanga mtawalia.

Mauzo haya yatafanyika Oktoba 27, 2016 katika chuo cha Taifa cha Utalii kampasi ya BUSTANI kilichopo katika makutano ya Mtaa wa Shaaban Robert/Samora Avenue mjini Dar es Salaam saa nne na nusu (4:30) asubuhi. Uuzaji huu utafanyika kwa njia ya makubaliano binafsi (private agreement) kwa kuzingatia kanuni 31 (iii) ya kanuni za sheria ya misitu za mwaka 2004. Miti hii ya misaji itauzwa mahali ilipo na jinsi ilivyo na mnunuzi hatakuwa na haki ya kudai fidia baada ya mauzo.

Downloads File: