Resources » News and Events

Jeshi la Polisi Mkoani Pwani kwa Kushirikiana na Maofisa wa Maliasili Wamekamata Viroba yya Bangi

Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Maofisa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) inamshikilia Dereva Bw.  Emanuel Bisama  (37) ambaye ni  mkazi wa Kimara Suka Dar es Salaam,kwa kosa la kusafirisha magunia mawili ya mkaa ambayo baada ya kupekuliwa ndani yake  kulikutwa na viroba viwili vyenye uzito kilo 50 kila kimoja vikiwa vimejaa bangi.

Akizungumza jana na Waandishi wa Habari  Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Pwani , ACP. Bonaventura Mushongi  alisema  Mtuhumiwa ambaye ni dereva wa  gari lenye namba za usajili T876 DDL  aina ya DAF Leyland  Bw. Emanuel Bisama (37) alikamatwa Septemba 21  saa 4.00 asubuhi  katika kata ya Vigwaza tarafa ya Chalinze mkoa wa Pwani katika Bara bara kuu ya Morogoro akitokea Tunduma na kwa sasa yupo mbaroni  kwa mahojiano licha ya kukana kuwa hakujua kilichomo ndani ya magunia hayo.

Kamanda Mushongi alisema walifanikiwa kumkamata wakiwa katika Operesheni ya Ukaguzi wa mazao ya Misitu katika Barabara kuu ya Morogoro hadi Dare Salaam, aliongeza kuwa Dereva huyo wa gari amefunguliwa kesi CHA/RB/3039/2016 kwa kosa la kupatikana na bangi.

Kwa upande Wakala wa Hudumza Misitu Tanzania (TFS) Kaimu wa Kanda ya Pwani Bw. Jonathan Mpangala alisema kuwa Mtuhumiwa huyo amefunguliwa kesi ya pili yenye CHA/RB/5113/2016 kwa kosa la kumiliki na kusafirisha mazao ya misitu bila kibali kwa sheria ya misitu namba 14 ya 2012 kifungu 88 na 89.

Alisisitiza kuwa Operesheni ya kukamata usafirishaji wa mazao ya misitu bila vibali itakuwa ya kudumu baada ya kuona magari mengi hasa makubwa yakiwa yamepakiwa magunia ya mkaa kuanzia mawili hadi matano ambayo yamekuwa yakioneka waziwazi hata ukiwa  barabarani namengi yakiwa hayalipiwa ushuru wa Serikali kuu na hata magari mengine yakiwa hayajalipiwa ushuru wa Halmashauri